Wednesday, 3 August 2016

PICHA 5 & VIDEO: Basi linalopita juu ya magari mengine lafanyiwa majaribio kaskazini mwa China

Siku kadhaa zilizopita ziliripotiwa taarifa za kutengenezwa kwa basi la umeme lenye uwezo wa kupita juu ya magari mengine huko China. Kutokana na China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi Duniani, hivyo basi hilo linatajwa kuwa ufumbuzi sahihi wa msongamano wa magari barabarani, imeelezwa kuwa basi hilo tayari limevutia serikali za Brazil, Ufaransa , India na Indonesia.

36D14DC600000578-3606602-image-a-28_1470177582302

Hii ndio mara ya kwanza kwa wabunifu hao kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuvuja katika mitandao mwezi May, wiki hii basi hilo limefanyiwa majaribio kwenye eneo la kaskazini mwa China jimbo la Hebei katika barabara iliyofanyiwa ukarabati yenye urefu wa mita 300, basi hilo lina uwezo wa kuhudumu kwa kasi ya kilometa 60 kwa saa na litakuwa na uwezo wa kubeba watu 1200 kwa wakati mmoja.

36D14DCB00000578-3606602-image-m-26_147017750605736D14DD200000578-3606602-image-a-19_147017746065136D14DD600000578-3606602-image-a-27_147017751410636D14DDA00000578-3606602-image-a-32_1470177737069

Unaweza kuangalia video hii hapa chini


No comments:

Post a Comment