Monday, 19 September 2016

Umeipata hii ya Kanye West kujiunga na Instagram leo? Nimekuwekea hapa.

Mtu wangu wa nguvu, ikufikie hii taarifa ya rapa mwenye vituko vya kila aina kwenye maisha yake, Kanye West kutoka nchini Marekani kujiunga na mtandao wa Instagram leo September 18, 2016.


Huenda ulikua hufahamu kama Kanye West hakua mtumiaji wa mtandao wa Instagram, kituo cha Tv cha Revolt kinachomilikiwa na rapa na mfanyabiashara Puff Daddy kimeripoti juu ya Kanye West kuingia rasmi kwenye mtandao wa Instagram unaotumiwa na watu wengi sana duniani. Kitu chakushangaza zaidi ni muda mfupi tu baada ya kujiunga na mtado huo, rapa Kanye West amepata zaidi ya Followers laki nne na ukurasa wake umekuwa Verified huku akiwa amepost picha moja tu. 

Mnamo tarehe 14 March 2016, Kanye West alitangaza kuwa atajiunga na mtandao wa Instagram lakini kwa mashari ambayo hakuyaweka wazi.

kanye-west-says-he-will-join-instagram-under-one-condition2

No comments:

Post a Comment