Tuesday, 20 September 2016

Messi amemtaja mchezaji bora zaidi yake… Utashangaa!!

Leo September 20, 2016 kwenye upande wa soka nimeipata hii ya Mshambuliaji was club ya BarcelonaLionel Messi ambaye amemtaja mchezaji anayemkubali zaidi duniani, najua utakua umeshaweka jina la mchezaji unayehisi Messi kamtaja mtu wangu.  

Mid fielder wa club ya Barcelona Andres Iniesta  ndiye mchezaji aliyetajwa na Messi kama mchezaji anayemkubali zaidi. Iniesta na Messi wote ni zao la Academy au Team B ya club ya Barcelona, Muajentina huyo amesema japokuwa wote wana mchezo unaofanana, Bado Iniesta mwenye asili ya Hispania amekuwa na uwezo wa kipekee ambao yeye binafsi amejikuta hawezi kuufikia.

>>>>Iniesta ni bora zaidi yangu, kila wakati namuona akiwa na mpira miguuni mwake. Ndivyo nimekuwa nikiuona ubora wake. Anafanya kila kitu kwa urahisi sana, kuna wakati anaonekana kama hafanyi kitu lakini ndio hapo anapofanya maajabu. Kila kitu ni tofauti kwa Andrés, unajua kitu kigumu kwenye football ni kufanya kila kitu kionekane rahisi tu, au hakitumii juhudi zozote, na hivyo ndo Andrés alivyo:– Messi

image

Mastaa hao wawili wamekua pamoja ndani ya Nou Camp tangu mwaka 2004 na kuisaidia club ya Barcelona kushinda mataji 8 ya ligi, manne kati ya hao ni ya Champions League huku manne yakiwa ni ya vikombe vya Copa Del Rey

No comments:

Post a Comment