Septemba 20 2016 kocha wa Man Cityya England Pep Guardiola ameweka wazi kwa nini hamchezeshi kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure, kocha huyo ambaye amejiunga msimu huu akitokea Bayern Munich ameandamwa na maneno kuhusiana na kuonesha dalili za kutomuhitaji nyota huyo.
Guardiola ametoa kauli katika vyombo vya habari kuwa Yaya Toure hawezi kuichezea tena Man City hadi atakapoomba radhi kwa wachezaji wenzake na timu kwa ujumla, kutokana na maneno yaliotolewa na wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk ambaye anamponda Guardiola amemdharirisha Toure kumuacha katika kikosi chaUEFA.
Pep Guardiola alitoa kauli kuwa “Toure ni lazima aombe radhi wachezaji wenzake, inabidi aombe radhi klabu kufuatia maneno yaliotolewa na wakala wake, kama hatofanya hivyo hatocheza” maneno hayo ya Guardiola aliyasema muda mchache baada ya Toure kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya Ivory Coast.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Toure ameshinda matajia 113 akiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast toka alipoanza kuichezea 2004 na ameshinda taji la mataifa ya Afrika 2015, ila Pep Guardiola anatajwa kutomuhitaji kiungo huyo kwani toka 2010 alisababisha nyota huyo akahama FC Barcelona na kujiunga na Man City.
No comments:
Post a Comment