Kila inapokaribia mwisho wa mwaka, kit up cha Televishen cha kimataifa MTV huwa kinaandaa list ya mastaa 10 wa muziki wa Hip Hop waliofanya vizuri zaidi, lakini mara nyingi list hiyo huwa na maswali mengi sana juu ya mastaa wanaotajwa kuwemo pamoja na aina ya uteuzi wa majina.
MTV’s Hottest MCs In The Game huandaliwa kwa kuwakutanisha watangazaji wa radio na tv kubwa za nchini Marekani na kwa mwaka huu ameshiriki pia mtangazaji staa “Charlamagne tha God”, kutoka kituo cha radio cha Power 105.1 FM, akiwa na crew ya watu wengine 8.
Kila wakati MTV wanapoachia list ya majina ya Rappers 10 wakali zaidi, huwa inasababisha watumiaji wa social networks kupandwa na hasira baada ya kutokubaliana na upangaji wa majina hayo. Na hiki ndicho kinachoonekana kutokea tena kwenye list hii.
Vigezo vya upangaji wa majina ya mastaa hawa huangaliwa kwa kutumia nguvu msanii kwenye vyombo vya habari, lebel inayomsimamia, pamoja na kura za majaji. Rapa mwenye kila aina ya mbwembwe, Kanye West ametajwa kuongoza list hiyo.
Nimeambiwa pia majina hayo 10 huchaguliwa kutoka kwenye list hi ya majina 40 ambayo huletwa mezani kwa majaji na kuanza kuipitia na kubakiza majina 10.
No comments:
Post a Comment