Baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye chart ya Billboard upande Albam bora za Hip Hop & R&B, Star anayeongoza kwa kufanya collabo zenye list ndefu ya wasanii nchini Marekani, DJ Khaled ameingia wenye headlines mpya baada ya single yake ya For Free kufikisha mauzo ya Platinum na kupewa tuzo na taasisi ya masuala ya burudani nchini humo ya RIAA(Recording Industry Association of America).
Alhamisi ya September 15, 2016, DJ Khaled aliandika kupitia Twitter na kueleza kuwa collabo yake na rapa kutoka YMCMB, Drake “For Free” imefikisha rekodi ya Platinum na kupewa tuzo ya RIAA.
Single hiyo, ilikuwa ya kwanza kuachiwa ndani ya albam yake ya tisa, Major Key, ilifanya vizuri kwenye chart za Billboard Hot 100 na kushika nafasi ya No. 13.
Hii sio mara ya kwanza kwa DJ Khaled kufikisha rekodi zake Platinum; single zake nyingine kama “I’m So Hood,” “I’m On One,” “All I Do Is Win,” “We Takin Over” na “I Wish You Would”zote hizi zilifanikiwa kupewa tuzo hiyo.
No comments:
Post a Comment