Daraja la kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi limezinduliwa hivi karibuni nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa futi 20 na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo chake ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.
Daraja hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie limezinduliwa July mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu hadi 800 kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.
No comments:
Post a Comment