Wednesday, 3 August 2016

VIDEO: Emirates imetua kwa dharura Dubai baada ya kushika moto angani


Ndege hiyo aina ya Boeing 777-300rubani alijua kuwa ina tatizo masaa matatu baada ya kupaa ikitokea uwanja wa ndege wa Trivandrum India na kutoa signal ya kuomba kutua kwa dharura, hadi sasa taarifa kutoka mirror.co.uk inaripoti kuwa hakuna mtu aliyeripotiwa kuumia.

Emirates na wataalamu wao bado hawajajua nini chanzo kilichosababisha ndege hiyo kushika moto, taarifa kutoka kwa msemaji wa Emirates inaeleza “Emirates inathibitisha kuwa ndege yao imepata ajali Dubai ikiwa inatokea India, ndege ilikuwa na abiria 282 na wafanyakazi 18 imetua kwa dharura dubai baada ya kushika moto”

CHANZO CHA HII STORI: mirror.co.uk


No comments:

Post a Comment