Diamond Platnumz Ijumaa hii ameitambulisha rasmi label yake ya ‘WCB’
pamoja na kumsaini Rich Mavoko mbele ya waandishi wa habari.
Rich Mavoko akisaini mbele ya Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa, Godfrey Mngereza
Aidha, Diamond alimtambulisha dada yake, Queen Darleen kuwa mmoja kati ya wasanii wapya wa label
hiyo.
Shughuli hiyo ilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa,
Godfrey Mngereza ambaye alizungumza na kumpongeza Diamond huku akiwataka
wasanii wengine kushirikiana kwa namna hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari katika hoteli ya Regency Park jijini
Dar es salaam, Diamond amesema WCB imemsani Rich Mavoko ili kuleta
chachu katika muziki.
“Nia ya kuwaita hapa ni kuonyesha kwamba wasanii tunaweza
kushirikiana, tunaweza kufanya kitu kikubwa, ni muda wa kuonyesha sio
ulimwengu wa vita kwa wasanii, watu wachukiane,” alisema Diamond.
“Tukishirikiana wasanii kwa wasanii tutaonyesha mfano bora kwa jamii na
hata mafanikio yataongezeka, kwa hiyo tuna Richard hapa na tunamshukuru
sana, karibu kwenye familia,” alisema Diamond.
Kwa upande wa Rich Mavoko ameshukuru kusainiwa na WCB, huku akiwaahidi mashabiki wake mambo mazuri
“Mimi nizishukuru media zote ambazo zimefika kwenye shughuli hii
maalum. Mimi nafikiri leo ni siku kubwa sana kwangu, kwa WCB pamoja na
kwa tasnia ya muziki kwa ujumla. Lengo letu kubwa ni kuonyesha kwamba
muziki wetu umefikia kwenye biashara kubwa sana, sisi tukionyesha umoja
hata serikali itaweza kutusupport. Kwa hiyo sisi wasanii wenyewe kwa
wenyewe tunabidi tuonyeshe undugu, pia serikali itaona sisi tupo serious
kwenye kazi, kwa hiyo lengo la kuwa na Nasib WCB ni kufanya naye kazi,
na naahidi kufanya kazi nzuri zaidi ili kufikisha muziki wetu sehemu
fulani,” alisema Rich Mavoko.
Pia Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza
ambaye alihudhuria shughuli hiyo, alimpongeza Diamond huku akiwataka na
wasanii wengine kushirikiana ili kuleta chachu kwenye muziki.
“Ni vizuri sana tunapo waona wasanii watanzania wanawekeza katika
industry ya muziki, kwa hatua hii inaondoa ile dhana kwamba wanaoweza
kuwekeza kwenye muziki ni watu toka nje, kwa hiyo ni hatua kubwa sana,
ni hatua ya msingi sana ambayo Diamond na team yake yote wameipiga
katika kuonyesha dhahiri kwamba kila kitu kinawezekana,” alisema
Mavoko ambaye pia amechia wimbo uitwao ‘Story’, amesaini mkataba wa miaka 10.
Pia mmoja kati ya mameneja wa WCB, Sallam alisema mkataba huo
haujamfunga Rick Mavoko kuondoka WCB, kama akihitaji kuondoka itabidi
anunue mkataba huo ndipo aondeke.
Diamond na Mavoko wakibadilishana mkataba
Diamond na Mavoko wakipongezana
Mavoko akisaini
Queen wa WCB
No comments:
Post a Comment