Thursday, 2 June 2016

Mwaka 2015 nilifanya kazi kwa hasara – Abydad

Mtayarishaji wa muziki anayefanya vizuri kwa sasa bongo, Abydad amekiri kufanya kazi kwa hasara mwaka 2015.


Abydad

Abydad ni miongoni mwa watayarishaji muziki wanaokuja kwa kasi baada ya kufanya nyimbo kadhaa zinazofanya vizuri kwenye redio ukiwemo ‘Nagharamia’, ‘Subira’, ‘Aje’ na nyingine kibao.

Akiongea kwenye kipindi cha ENews, kinachoruka kupitia EATV, Abydad alisema, “Kitu cha kwanza mwaka jana nilipanga kujitambulisha kwenye muziki vizuri nilipanga nijulikane, hivyo ili utambulike ilikuwa ni lazima nitafute wasanii wakubwa ili nifanye nao kazi nashukuru hilo nilifanikiwa. Hivyo nilifanya kazi na wasanii wakubwa lakini kihasara hasara ili niweze kufikia malengo, lakini kwa sasa nafanya kazi na mwaka 2016 nimeanza na kazi mpya ya Alikiba ‘Aje’ zinakuja zingine kali sana naweza kusema kuwa sasa kazi imeanza 2016.”

No comments:

Post a Comment