Baada ya kupoteza mchezo huo ambao ulikuwa wa tatu baada ya kupoteza dhidi ya Man City katika dimba la Old Trafford kwa goli 2-1 na kupoteza dhidi yaFeyenoord katika mchezo wa Europa League kwa goli 1-0, presha mitandaoni iliendelea kumuandama Paul Pogbaaliyenunuliwa kwa dau kubwa na kuweka rekodi ya usajili.
Kiungo huyo wa Ufaransa ambaye hajafanya vizuri bado akiwa na Man United toka avunje rekodi ya usajili alitumia account yake rasmi ya instagram kuandika ujumbe kwa mashabiki “Asante kwa mashabiki wote kuwa pamoja na sisi matokeo bado sio mazuri kwa upande wetu, lakini tunaendelea kupambana, Man United tunaweza”
No comments:
Post a Comment