Mtoto wa miaka 10 kutoka Indonesia, ambaye ametajwa kuwa mtoto aliyenenepa zaidi duniani alianza kupewa chakula cha kupunguza uzito Arya Permana ameorodheshwa kuwa na unene usio wa kawaida kwa kuwa alikuwa na uzani wa kilo 188.
Mtoto huyu hatimaye ameweza kurudi shuleni baada ya kupunguza uzito wa kutosha wa kumwezesha yeye kutembea kwani siku zote alikuwa akillala na hakuweza kutembea na kusababisha yeye kukatisha masomo.
Mtoto huyu unaambiwa amekuwa akila milo mitano kwa siku lakini baada ya ushauri wa kufanya diet na mazoezi makali Arya ameanza kupunguza uzito ndani ya wiki chache sasa anaweza kukaa lakini pia kutembea kwenda shule na kucheza na wenzake darasani
No comments:
Post a Comment