Tuesday, 5 July 2016

Bei za tiketi kwa watakaoenda kuangalia kombe la dunia 2018

Michuano ya Kombe la dunia 2018 itakayofanyika Urusi inakaribia kuanza kwani bado mwaka mmoja na miezi kadhaa, kwa kawaida Kombe la dunia hufanyika kila baada ya miaka minne, hivyo kama una mpango wa kwenda kuangalia mechi za Kombe la dunia 2018, ninazo bei za tiketi.

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFAlimeripotiwa na 101goals.com kutaja bei za tiketi za michuano hiyo itakayoanza 2018, bei ya tiketi ya michuano hiyo itaanzia dola 105 kwa raia wa kigeni ambazo ni zaidi ya Tsh 230,000, lakini bei ya tiketi za fainali ya michuano hiyo inatajwa kuwa itafikia dola 1100 ambazo ni zaidi ya Tsh milioni 2.4.

FIFA-crooks-Russia-1024x512

Mgawanyiko wa bei za tiketi za fainali za michuano hiyo kwa mwaka 2018

Kwa watu ambao makazi yao ni Urusibei ya tiketi hizo kwa kima cha chini watauziwa dola 20 ambazo ni Tsh 40,000.

No comments:

Post a Comment