Hakuna jibu zuri la jambo la mzaha kama lenye mzaha pia.
Hivi karibuni gazeti moja la udaku liliwachora mastaa wa kike wenye
uhusiano na mastaa wa Bongo wanaowazidi umri. Mastaa hao ni pamoja na
Jacqueline Wolper aliyechorwa akimnywesha uji mpenzi wa Harmonize
anayeonekana akiwa amebeba mdoli.
Wengine ni Wema Sepetu akiwa amempakata Idris Sultan, Zari the
Bosslady akimweka Diamond kwenye kitolori cha kuwafundishia watoto
kucheza na Aunty Ezekiel akiwa amembeba mgongoni mpenzi wake Mose Iyobo.
Ni Wema pekee ndiye aliyeijibu kwa kupost picha hiyo kwenye akaunti yake na kuandika: Aliechora
hii natamani tu nimuone… Nimpe mkono. Leo nimeongeza siku za kuishi
wallahy…. I jus laughed too much today….. Ukisoma na dialogue ndo
unakufa kabisa…. Nimeipenda hio ya “Aogopa Mimi… Aogopa chacha.”
No comments:
Post a Comment