Saturday, 17 December 2016

MTV wameniletea haya majina 10 ya "Hottest MC's" waliofanya vizuri 2016 (+List&Picha)

 

Wednesday, 12 October 2016

VIDEO: Dogo wa miaka 10 kasajiliwa na Juventus anatabiriwa kuwa kama Messi

img_5947-1

Rashed Al Hajjawi ambaye video yake imeonekana katika mitandao hivi karibuni Juventus wameonesha dhamira ya dhati ya kuanza kuhitaji huduma ya mtoto huyo ambaye anatazamiwa kuja kuwa kama mshambuliaji wa FC Barcelona Lionel Messi.


Thursday, 22 September 2016

Taarifa nzuri kwa mashabiki wa Davido, Sony Music kuachia kazi zake soon!!


imageKimya cha takribani miezi kumi na moja cha msanii Davido huenda kikamalizika siku chache kutoka sasa, Hii ni baada ya star huyo anayesimamiwa kazi zake na lebel ya RCA records iliyoko chini ya Sony Music, kupost video akiwapa taarifa kuanza kuachiwa video zake zaidi ya 20 kabla mwaka 2016 haujaisha.

Davido kupitia video hiyo amesema anapanga kwa kuumaliza mwaka 2016 kwa style tofauti ili afanane na label yak, Sony Music ambao amedai kuwa wamemruhusu kuanza kuachia kazi zake ikiwemo albam yake mpya itakayoitwa Son of Mercy, ambayo itatoka ndani ya mwaka huu.

Davido alisaini deal ya usimamizi wa kazi zake na kamouni ya Sony Music, January 20 2016 ambapo Taifa la Nigeria lilikua taifa la kwanza barani Afrika kuingia makubaliano hayo na kuwa msanii wa kwanza wa Afrika kutia saini ya record deal hiyo.

Mtazame Davido akiongelea hilo hapa chini.


Tuesday, 20 September 2016

Alichozungumza Obama kwenye hotuba yake ya mwisho mkutano wa UN

Kupitia hotuba aliyoitoa Rais wa Marekani Barack Obama ameyataka mataifa tajiri kufanya kila linalowezekana kuwasaidia watu wanaokimbia vita huku akikiri kuwa dunia inakabiliwa na changamoto nyingi na kuzitaka nchi tajiri kuchukulia tatizo hilo kama ni lao huku akisema kuwa ongezeko la wakimbizi ni ishara ya vita na mateso na kwamba hali hiyo itaweza kushughulikiwa tu endapo migogoro kama ule wa Syria itamalizwa.0c839261-8851-40b9-82b4-71392a9079fd_w987_r0_s

Huu unakua mkutano wa mwisho kwa viongozi wakubwa wawili ambao ni Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambao wanahudhuria vikao hivyo kwa mara ya mwisho wakiwa madarakani. 



Septemba 20 2016 kocha wa Man Cityya England Pep Guardiola ameweka wazi kwa nini hamchezeshi kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Yaya Toure, kocha huyo ambaye amejiunga msimu huu akitokea Bayern Munich ameandamwa na maneno kuhusiana na kuonesha dalili za kutomuhitaji nyota huyo.

Guardiola ametoa kauli katika vyombo vya habari kuwa Yaya Toure hawezi kuichezea tena Man City hadi atakapoomba radhi kwa wachezaji wenzake na timu kwa ujumla, kutokana na maneno yaliotolewa na wakala wa mchezaji huyo Dimitri Seluk  ambaye anamponda Guardiola amemdharirisha Toure kumuacha katika kikosi chaUEFA.

pep-guardiola-617582

Pep Guardiola alitoa kauli kuwa “Toure ni lazima aombe radhi wachezaji wenzake, inabidi aombe radhi klabu kufuatia maneno yaliotolewa na wakala wake, kama hatofanya hivyo hatocheza” maneno hayo ya Guardiola aliyasema muda mchache baada ya Toure kutangaza kustaafu kucheza timu ya taifa ya Ivory Coast.

download

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Toure ameshinda matajia 113 akiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast toka alipoanza kuichezea 2004 na ameshinda taji la mataifa ya Afrika 2015, ila Pep Guardiola anatajwa kutomuhitaji kiungo huyo kwani toka 2010 alisababisha nyota huyo akahama FC Barcelona na kujiunga na Man City.

Messi amemtaja mchezaji bora zaidi yake… Utashangaa!!

Leo September 20, 2016 kwenye upande wa soka nimeipata hii ya Mshambuliaji was club ya BarcelonaLionel Messi ambaye amemtaja mchezaji anayemkubali zaidi duniani, najua utakua umeshaweka jina la mchezaji unayehisi Messi kamtaja mtu wangu.  

Mid fielder wa club ya Barcelona Andres Iniesta  ndiye mchezaji aliyetajwa na Messi kama mchezaji anayemkubali zaidi. Iniesta na Messi wote ni zao la Academy au Team B ya club ya Barcelona, Muajentina huyo amesema japokuwa wote wana mchezo unaofanana, Bado Iniesta mwenye asili ya Hispania amekuwa na uwezo wa kipekee ambao yeye binafsi amejikuta hawezi kuufikia.

>>>>Iniesta ni bora zaidi yangu, kila wakati namuona akiwa na mpira miguuni mwake. Ndivyo nimekuwa nikiuona ubora wake. Anafanya kila kitu kwa urahisi sana, kuna wakati anaonekana kama hafanyi kitu lakini ndio hapo anapofanya maajabu. Kila kitu ni tofauti kwa Andrés, unajua kitu kigumu kwenye football ni kufanya kila kitu kionekane rahisi tu, au hakitumii juhudi zozote, na hivyo ndo Andrés alivyo:– Messi

image

Mastaa hao wawili wamekua pamoja ndani ya Nou Camp tangu mwaka 2004 na kuisaidia club ya Barcelona kushinda mataji 8 ya ligi, manne kati ya hao ni ya Champions League huku manne yakiwa ni ya vikombe vya Copa Del Rey

Monday, 19 September 2016

Mchekeshaji Kevin Hart amerudi kwenye game ya muziki?

Najua wengi mtakuwa mnamfahamu mchekeshaji mkubwa na maarufu duniani kutokea Marekani Kevin Hart, amezikamata headlines kwenye mitandao mbalimbali kwa uamuzi wake wa kurudi kwenye Game ya muziki wa Hip hop ambapo apo awali alisitisha na kujikita kwenye fani ya uchekeshaji zaidi.

Kituo kikubwa cha Marekani Enewskimeripoti kuwa Kevin Hart  a.k.a Rapper Chocolate Droppa jina analolitumia kimziki ambapo Leo September 19 2016 ameachia single iliobeba jina “Baller Alert” chini ya studio Motown Records za Marekani.

rs_640x962-160914160506-640-kevin-hart-chocolate-droppa-bn-091416

Zaidi anatarajia pia kutoa mixtape yake ya What now? atakayoiachia Oct 7, pia nakusogezea video Kevin Hart a.k.a Chocolate Droppa akiwa ana chana free style, itazame hapa chini mtu wangu