Sunday, 11 September 2016

Rais Magufuli kaahirisha ziara yake ya kwenda Zambia.

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu ya kwenda Zambia ambapo pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa sita wa Zambia Edgar Chagwa Lungu.

Rais Magufuli amechukua huo uamuzi ili aweze kushughulikia madhara ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu  16, mamia wakiwa wamejeruhiwa na nyumba kadhaa kubomoka Kagera.

Rais Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha ambapo sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa sita wa Zambia zinatarajiwa kufanyika tarehe 13 September 2016 kwenye mji wa Lusaka.

No comments:

Post a Comment