Sunday, 11 September 2016

Baada ya Kudaiwa Anavaa Cheni Feki..Jack Wolper Aonyesha Cheni zake za Dhahabu


Malkia wa filamu Jacqueline Wolper amewaziba mdomo wanaomsema anavaa cheni fake za dhahabu.

Mwigizaji huyo ambaye kwa sasa yupo kwenye mahaba mazito na Harmonize, amesema kwa sasa hataki kuonyesha vitu kama hivyo kwa kuwa wakati wake wakufanya hivyo ulishapita.

“Stylish flevaaaa zone msioneane wivu nikiwa tajiri nitaweka kila mmoja sehemu yake wanangu sawa madinizii. Sema mimi mswahili sana najipenda navyowashuhulikia waswahili wenzangu kwa maneno yao yakutunga, msinifanye niwe naonyesha paka nachokula kila siku maana naweza pia,” aliandika Wopler Instagram.

Aliongeza,

“Angalieni maisha yenu, kwahyo tusipofanya show off sio hatuna, vingine tunawaachia chipukizi jamani sahivi tunatakiwa tuonyeshe magorofa . Stay tune Mazafokoooziii delivere,”

Kwa sasa mwingizaji huyo amejikita zaidi kwenye biashara kuliko katika kuzalisha filamu.

No comments:

Post a Comment