Hit maker wa Shikorobo, Shetta Alhamisi hii aliandaa sherehe maalum
ya kuwashukuru mashabiki wa muziki wake kwa kumfikisha hapo alipo pamoja
na kuitambulisha management yake mpya.
Shetta akimtambulisha baunsa wake, anaitwa Mbrazili
Sherehe hiyo ambayo iliambatana na uzinduzi wa management ya Shetta,
ilipambwa na mastaa mbalimbali wa muziki, filamu pamoja na wadau wa
sanaa ya muziki.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika sherehe hiyo
iliyofanyika katika ukumbi wa Rouge Hyatt Recency Hotel, Jijini Dar es
salaam, Shetta alisema ameamua kufanya hivyo ili kuwashukuru wadau
mbalimbali waliomsaidia kumfikisha hapo alipo.
“Kusema kweli Shetta amekuwa na safari ndefu katika maisha yake ya
muziki, lakini haya mafanikio yamekuja kwa michango ya watu wengi sana,
media, mashabiki pamoja watu wangu wa karibu. Kwa hiyo nimeona bora
niwaite hapa ili tujipongeze kwa hapa tulipofikia, kwa sababu haikuwa
kazi rahisi. Hapa nimewaalika watu mbalimbali pamoja na mashabiki wangu
ili waje na wao kufurahia hapa nilipofikia, kwa hiyo tutakumwa na kula
pamoja,” alisema Shetta.
Pia Shetta aliweza kutambulisha management yake mpya, baunsa wa kumlinda pamoja na dancer. Angalia picha.
Shetta akitambulisha management yake mpya ikiongozwa na Michael Mligwa aka MxCarter (wakati kati)
Idris akiongea na waandishi wa habari
Idris Sultan
Irene Uwoyo
Linah akiwa katika pozi
Mashabiki wa Shetta wakisikiliza jambo kwa makini
Master Jay akiwa na Alawi Junior
Shaa
Shetta na Barnaba
Shetta akimtambulisha baunsa wake
Shetta akiwa na Gadner
Shetta akiwa red carpet
Shetta akiwasili eneo la tukio
Shetta akiwatambulisha dancer wake
Shetta akizungumza
No comments:
Post a Comment