Headlines za kocha wa Man UnitedLouis van Gaal kuwa huenda taondoka klabu hapo zimekuwa zikichukua nafasi kila siku, kwani mashabiki wa timu hiyo hawana imani na uwezo wa kocha huyo tena, baadhi ya wachezaji wanahusishwa kuwa hawauelewi mfumo wa kocha huyo ukilinganisha na wakati ambao yupo Sir Alex Ferguson.
Stori za Van Gaal kuhusishwa kufukuzwa kazi zimekuwa zikiandikwa ila December 5 kabla ya mchezo kati ya Man United dhidi ya West Ham UnitedLouis van Gaal katoa majibu ya kuhusu hatma yake ndani ya Man United. Van Gaal yupo radhi kuondoka Man Unitedendapo tu wachezaji wataamua aondoke.
“Mimi ndiye kocha wa kwanza ambaye huwa naachia ngazi na hilo linathibitisha kupitia klabu nilizofundisha pia kazi nilizozifanya, sidhani kama kuna kocha yeyote ambaye huwa anaondoka mwenyewe tu au sababu ya pesa, ila mimi nipo hivyo”>>> Van Gaal.

No comments:
Post a Comment