Jumamosi ya December 5 Ligi Kuu Uingereza imeendelea tena kwa michezo nane kupigwa, mchezo wa kwanza kupigwa ulikuwa ni mchezo kati ya Stoke City dhidi ya Manchester Citykatika dimba la Britannia lenye uwezo wa kuchukua mashabiki 28383. Huu ulikuwa ni mchezo muhimu kwa Man City ambao wanamipango ya kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi.
Man City ambao walikuwa na point 29 kabla ya mchezo huu kuchezwa, walianza kwa kuruhusu kufungwa magoli mawili ya haraka, kitendo ambacho kilifanya mchezo kuzidi kuwa mgumu kwa Man City, kwani baada ya Stoke Citykuongoza kwa goli 2-0 hadi dakika ya 80 walianza kuwa makini na ulinzi wa magoli yao hili yasirudishwe na Man City.
Mchezo ulimalizika kwa Man City ambao wapo kileleni mwa Ligi Kuu kwa muda. kwani uwezekano wa wao kuendelea kusalia kileleni kunategemea matokeo ya mechi za Leicester City, Man United na Arsenal. Mchezo wa Man City na Stoke City ulimalizika kwa Stoke kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na Marko Arnautovic dakika ya 7 na 15.
Video ya magoli ya Stoke City Vs Man City


No comments:
Post a Comment