Miongoni mwa ile michezo 9 ya LaLigaya weekend hii, tayari baadhi ya michezo hiyo imeshachezwa Jumamosi ya December 5, miongoni mwa mechi za Ligi ya Hispania zilizochezwa ni mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Getafe, mechi ambayo ilikuwa inapewa nafasi Real Madrid kushinda na kupunguza tofauti ya point dhidi ya FC Barcelona.
Real Madrid ambayo ilikuwa na utofauti wa point 6 dhidi ya FC Barcelona, imeikaribisha Getafe katika dimba la Santiago Bernabeu na kuifunga jumla ya goli 4-1 na kufanya itimize jumla ya point 30 na michezo 14 ikiwa ni tofauti ya point tatu dhidi ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona.
Magoli ya Real Madrid yalianza kufungwa na Karim Benzema dakika ya 4 na 16, Gareth Bale dakika ya 35 kabla ya Cristiano Ronaldo kufunga goli la nne dakika 38. Getafe walirudi kipindi cha pili kutafuta magoli ya kusawazisha, jitihada ambazo ziligonga mwamba na kuambulia goli moja pekee lililofungwa na Alexis dakika ya 70.
Video ya magoli ya Real Madrid VsGetafe


No comments:
Post a Comment