Monday 12 September 2016

Alikiba kutumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA, Oktoba 22

Muimbaji wa Aje, Alikiba ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo za MTV MAMA huko Johannesburg, Afrika Kusini.
ddddd
Kupitia mtandao wa Instagram wa meneja wa msanii huyo, Seven Mosha ameweka picha ya msanii wake huyo na kuandika ujumbe unaosomeka, “The King @officialalikiba is set to perform at the MTVAfrica Music Awards 2016 .”
Pia MTV Base wameandika: Yes,@OfficialAliKiba to bring that HEAT to the stage 

Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Ticketpro Dome, Jumamosi ya Oktoba 22, mwaka huu. Wasanii wengine wanaotarajia kutumbuiza kwenye tuzo hizo ni pamoja na Yemi Alade, Nasty C, Babes Wodumo na wengine wengi. Kwa mwaka huu tuzo hizo zina vipengele 18 ambavyo wasanii kutoka nchi mbalimbali za Afrika watawania.

No comments:

Post a Comment