
Akiongea kwenye 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM, Bella ambaye hivi karibuni amekuwa kimya kiasi, amedai kuwa yeye kama mmiliki wa bendi hiyo amejiwekea utaratibu wa kuhakikisha brand yake inakuwa juu zaidi kuliko bendi.
“Hiyo style siwezi kuja kuibadilisha, mimi naweka kipaumbele Christian Bella kwanza, hamzijui tabia za wasanii na sitaki watu wote wafuate mfano wangu, hatuwezi kufanana bendi zipo nyingi, Akudo watafanya kama Akudo,” amesema.
“Mimi style yangu ni Christian Bella kwanza mbele nalinda kwanza jina la Christian Bella. Mimi najibrand kwanza, mtasema huyu jamaa mbinafsi, ni mimi, hiyo ni style yangu, siwezi kuishi nikufurahishe wewe, najifurahisha mimi, nataka nilinde UChristian Bella mwisho wa siku niwe na uwezo wa kuwa mimi. Mimi bendi yangu natoa nao ngoma mpaka mimi niamue,” amesisitiza.
Muimbaji huyo anadai kuwa anafanya hivyo ili hata kama mtu akiondoka kwenye bendi yake kusionakane pengo lolote.
Katika hatua nyingine muimbaji huyo anatarajia kufanya show yake ya aliyoipa jina ‘Miaka 10 Kwenye Game TZ’ June 4.
“Ni baada ya miezi kazaa sijaonekana stejini
Dar es salaam Sasa nawakaribisha tarehe 04/June /2016 itakua Jumamosi ijao, tutasherekea miaka 10 ya C.B kwenye game tz, mnipongeze kwa machache niliofanya kwenye game tz,” aliandika kwenye Instagram.
No comments:
Post a Comment