Thursday, 2 June 2016

Mirror asema haya baada ya kuambiwa alitakiwa kuwa mbali kimuziki lakini anafanya muziki kwa kurelax


Msanii wa muziki ambaye yupo chini ya kampuni ya Wema Sepetu ‘Endless Film’, Mirror, amesema ni kweli anafanya muziki kwa kurelax kama watu wanavyodai kwa kuwa hali hiyo inampatia nafasi nzuri ya kufanya muziki mzuri na unaodumu kwa muda mrefu.
Mirror_full

Akiongeza na Bongo5 Jumapili hii, Mirror amesema kufanya kazi kwa kurelax hakucheleweshi mafanikio yake, bali kunampatia nafasi ya kufanya muziki mzuri.

“Muziki hauhitaji kukurupuka, unahitaji kurelax katika kuandaa kazi, ndio maana wale ambao wanaona mimi nafanya muziki kwa kurelax, nataka niwaonyeshe nilikuwa nafanya nini, na pia kwenye game bado nafanya vizuri toka nimenza” alisema Mirror.

Mirror ambaye anajipanga kuachia kazi yake mpya na Ommy Dimpoz, amesema hali ya kufanya muziki kwa kurelax kunamsaidia msanii kukaa kwenye chati kwa muda mrefu bila kutetereka.

No comments:

Post a Comment