
Hivyo hivyo hata kwa Mkubwa Fella, bila yeye siamini hata kama kungekuwa na Yamoto Band, Chege na Temba na TMK Family kwa ujumla.
Tuna wasimamizi wengi sana wanaowameneji wasanii lakini ukija kuwazungumzia Tale na Fella huko unakuwa umegusa nguzo tegemezi za meziki wetu ambao tunamshukuru kwa hapa tulipofikia huenda wakajitokeza wasimamizi wengi na wenye mapenzi kama yao.

Sandu George aka Kidboy
Sandu George Mpanda maarufu sana kwa jina la Kidboy ni mmiliki wa studio ya Tetemesha Records, mwandishi wa habari na pia ni mtangazaji wa zamani wa Radio Free Africa ambaye kwa sasa ni program manager wa kituo kipya cha radio, Lake FM iliyopo jijini Mwanza.
Kid naye ana historia yenye ukubwa wa aina yake katika muziki huu wa kizazi kipya kwani naye ni miongoni mwa wasimamizi wazuri wa wasanii.
Kidboy amekuwa ni prodyuza wa muda mrefu na kufanya kazi na wasanii wakongwe katika game ya Bongo Flava mfano Joh Makini amesha gonga ngoma kama mbili hivi Tetemesha ambazo ni Matawi na Sitochoka aliyomshirikisha Farida muimbaji wa kike kutoka Mwanza.
KID alianza kuibariki Tetemesha kwa kumsimamia msanii wa kwanza aitwaye Hussein Machozi aliyeteka hisia za watu wengi sana na kupelekea kuwa kipenzi cha watu kila kona kutojana na uimbaji wake wenye hisia.
Machozi alisumbua chati mbalimbali na kufikia hatua ya kuingiza nyimbo mbili katika chati moja na Kidboy.
Alifanikiwa kumtafutia collabo na msanii mkubwa kutoka Kenya DNA katika ngoma ya Full Shangwe iliyokuwa na version mbili na ile ya AY.
Hussein alitengeneza hit nyingi sana ikiwemo Kwaajili Yako, Utaipenda, Kafia Ghetto, Promise na Za Mwizi 40.
Kutokana na usimamizi mzuri uliompa umaarufu ndani na nje ya Tanzania, Hussein machozi aliamua kutoka katika uongozi wa Tetemesha na kujisimamia mwenyewe ambapo hakudumu kwa muda kwenye gemu na kupelekea kutangaza kuachana na muziki hivi karibuni.
Kete ilivyotoka kwa Hussein ilienda direct kwa kijana mdogo Sajna, msanii kutoka Mwanza aliyepata nafasi ya kusimamiwa na mtangazaji huyo wa, Showtime kipindi hicho RFA.
Sajna alikuja vizuri sana na aliibuka ghafla kama Tsunami na Tanzania nzima wakampokea. Aliwashangaza wengi kwani alikuwa anafanya poa huku akiwa bado yupo shule.
Hitmaker huyo wa Iveta asingekuwa maarufu kama asingekuwa katika usimamizi wa menejimenti yenye connection nzuri zaidi katika media mbalimbali. Tutazidi kummiss Sajna na kazi zake za Mganga na Iveta na Sitaki Kuumizwa aliyomshirikisha Linah ambazo ni miongoni mwa ngoma zilizomtambulisha katika game.
Kid hakuchoka kusapoti vipaji vya nyumbani hasa kwa mkoa wa Mwanza ambako kumekuwa na ukosefu wa wasanii wanaoimba. Tetemesha ilimsaini msanii mwingine tena, Csir Madini. Kama kawaida ya Kidboy ni kuwatengeneza mastaa kutokana na userious wake katika kazi.
CSir alibisha hodi na Kifungo Huru na kufunguliwa mlango. Wengi walimsifia kwa uandishi wake. Hakudumu Tetemesha kama wenzake lakini kwa kipindi chote alipokuwa Tetemesha alitengeneza hit takribani tatu zikiwemo Nishike Mkono, Kifungo Huru na Pain Killer.
Baada ya CSir kuachana na Tetemesha msimamizi huyo alikaa kimya kwa kipindi na akahamisha studio zake kutoka Mwanza na kuzileta jiji Dar. Kwakuwa mapenzi ya muziki yapo katika damu yake, alivunja ukimya tena na kutuletea kipaji kingine tena kutoka rock city, Barakah Da Prince.
Alirudisha furaha ya Kid na kuyasahau yote yaliyotokea kwa wasanii aliowasimamia hapo awali. Jichunge ndiyo track ya kwanza kwa Baraka chini ya Tetemesha.
Njaa ya Barakah ilimpa morali Kidboy kwa kutanua wigo wa msanii wake na kumpush nje na kufanikiwa kuchezwa kazi zake MTV na Trace TV.
Haikuwa rahisi kwa Barakah kufikisha kazi zake huko bila ya juhudi za Kid aliyemtengeneza Barakah na kuwa brand inayotolewa macho na wadau mbalimbali wa muziki. Kubwa zaidi Kid amemuachia alama ya tuzo ya msanii chipukizi mwaka 2015, hitmaket huyo wa Siwezi ambaye kwa sasa hayupo tena na Kidboy.
Hata hivyo kwenye mikono ya Kid, Barakah aliachia hits zingine mbili zikiwemo Siachana Nawe na Nivumilie alioshirikishwa Ruby.
Nguvu na jitihada zake Kidboy ndizo zinachompa nafasi ya kuketi meza moja na Tale au Fella ambao wanaliendesha gurudumu la burudani nchini.
No comments:
Post a Comment