Thursday, 2 June 2016

Kesi ya Messi na baba yake imeanza kusikilizwa tena Mahakamani jiji la Barcelona

Mchezaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi na baba yake mzazi Jorge Messi wanatuhumiwa kwa kosa la ukwepaji kodi na May 31 2016 inaripotiwa kesi yao imeanza kusikilizwa katika jiji la Barcelona Hispania.


34CA070800000578-0-image-a-2_1464697193033-1

Messi ni mchezaji bora wa dunia mara tano, kesi inayomkabili ya ukwepaji kodi wa Pound milioni 3.2 ambazo ni zaidi ya bilioni 10 za kitanzania imeanza kusikilizwa.

Messi na baba yake, walikwepa kulipa kodi hiyo kati ya mwaka 2007 na 2009 wakati mauzo ya picha za staa huyo wa FC Barcelona, ofisi ya waendesha mashtaka wamependekeza Lionel Messi na baba yake wahukumiwe miezi 22 jela.

No comments:

Post a Comment