
Akiongea katika kipindi cha Take One cha Clouds TV Jumanne hii, Wolper amesema Harmonize anaonyesha ni mtu ambaye ameshatendwa sana hivyo hataki tena hali hiyo imrudie.
“Harmonize ana hofu ya mungu, ni muoga kuumizwa sana, sijui waliyopita ilikuwaje?, lakini anasema anaogopa sana kuumizwa hicho ndio kitu ambacho kinanifanya niogope kabisa kufanya kitu chochote kibaya, yaani ni muoga wa kuumizwa kuliko kitu chochote,” alisema Wolper.
Muigizaji huyo amesema Harmonize ameweza kumsahaulisha mambo yote aliyofanyiwa na Mkongo kwa muda mfupi.
Pia amewataka mashabiki wake wa filamu kuacha kumtukania mpenzi wake huyo, kwani ni bora atukanwe yeye.
No comments:
Post a Comment