Thursday, 2 June 2016

Game ya muziki imekuwa tamu kama kipisi cha keki – Ibra Da Hustler

Rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Ibra Da Hustler amesema game ya muziki imekuwa tamu kama kipisi cha keki kwa kuwa linalipa zaidi kuliko zamani hali ambayo inampa machungu ya kufanya kazi kwa bidii.

Ibra Da Hustler

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, Ibra Da Hustler amesema anafurahi kuona wasanii kama Ali Kiba wasainiwa na Sony.

“Muziki kwa sasa umefikia sehemu nzuri sana, yaani game ya muziki imekuwa tamu kama kipande cha keki, wasanii wanalipwa vizuri sana tofauti na ule wakati wetu,” alisema Ibra Da Hustler. “Ndio maana najipanga kurudi ili kulichangamsha game zaidi, kwa sababu bado naamini mashabiki wangu wanapenda muziki wangu,”

Rappa huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa kolabo yake na G. Nako.

No comments:

Post a Comment