Thursday, 2 June 2016

Country Boy asema hajawahi kumuona Young Dee akitumia Madawa ya kulevya lakini…

Rapa Country Boy amesema hajawahi kushuhudia rafiki yake wa zamani Young Dee akitumia Madawa ya kulevya.

Young D na Country Boy

Young Dee amekuwa akikanusha mara kadhaa taarifa ya kutumia Madawa ya kulevya lakini bado amekuwa akiandamwa na maswali mengi kuhusu matumizi yake.

Akiongea na Bongo5z Country Boy ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Young Dee, amesema hajawahi kushuhudia rafiki yake huyo akitumia Madawa ya kulevya lakini kama anatumia basi atakuwa anamuheshimu sana ndio maana hajawahi kumuonyesha dalili yoyote.

“Young Dee nimekaa naye kwa muda mrefu kiukweli, kusema kweli kabisa sijawahi muona akitumia,” alisema Country Boy. “Maneno yapo na kila kitu kinatokea na kila kitu kinasikika, kama ni kweli anatumia basi nahisi alikuwa ananiheshimu sana, kwa sababu ni mwanangu nimekaa naye pamoja kwa muda mrefu sijawahi kuona kitu chochote kibaya zaidi tu ya ulevi wa kawaida, pombe tu,”

Aliongeza, “Lakini hiki kitu sio vizuri kwa mtu yeyote yule, kwa sababu hakina faida yoyote zaidi ya kukupoteza,”

Country Boy na Young Dee kwa sasa sio washikaji kama zamani, kwa wawili hao walipishana lugha baada ya Young Dee kujiondoa katika Kundi la ‘Mtu Chee’ ambalo lilikuwa linaundwa na Young Dee, Stamina pamoja na Country Boy.

No comments:

Post a Comment