Muziki wa Africa kwa sasa ni muziki unaosikilizwa na kufuatiliwa na watu wengi sana duniani tukiacha Waafrika wenyewe. Miezi kadhaa iliyopita tumeshuhudia wasanii kama Swizz Beats na Alicia Keys wakipost video zao kwenyeInstagram wakiwa wanacheza ngoma za wasanii kutoka Africa kama Wizkidna Diamond Platnumz.
Leo nimekutana na tweets za rapper kutoka South Africa, AKA zinazo washambulia wale wote wanaomuuliza lini atafanya kazi na wasanii wakimataifa, unajua jibu lake lilikuaje..? Kikubwa alichokigusia AKA kwenye tweets zake nne ni pamoja na kusema “kufanya collabo za kimataifa sio mpaka ufanye na wasanii wa nje ya Africa..!“
AKA amesisitiza kufanya collabo na wasanii kama Diamond Platnumz, Wizkid na Burnaboy wa Nigeria tayari ni collabo za kimataifa! Na kama wewe ni mmoja ya wale wanaoamini kuvuka mipaka ni kuimba na msanii wa Marekani basi chukua hii #tip kutoka kwa AKA kwenye hizi tweets zake nne hapa chini..
Mpaka sasa AKA amesharekodi wimbo na Diamond Platnumz pamoja na kufanya feature kwenye single mpya ya Joh Makini ‘Don’t Bother’.





No comments:
Post a Comment