Thursday, 2 June 2016

Sony Music waanza kuchekelea mafanikio ya Alikiba

Sony Music wameanza kuona matunda ya kumsainisha Alikiba ndani ya wiki moja tu.
13248676_474079762796293_792588935_n

Video ya wimbo mpya wa staa huyo, Aje, imefikisha views milioni 1 ndani ya siku saba tangu iwekwe kwenye mtandao wa Youtube.

Hiyo haijawahi kutokea kwa msanii yeyote wa Afrika aliyefikisha idadi hiyo ya views ndani ya wiki moja akiwa chini ya label hiyo.

Ndio maana hawakusita kujivunia kwa hatua hiyo.

“In 1 week, @OfficialAliKiba’s music video for #AJE, has hit 1mil views! Nice one, Africa! Keep going,” wameandika Sony kwenye Twitter.

No comments:

Post a Comment