Monday, 7 December 2015

Vitu vitano vya kufahamu kuhusu staa wa muziki, Shakira..!

Najua nina watu wangu ambao ni mashabiki wakubwa wa muziki wa Shakira na style zake za kucheza… licha ya kutengeneza jina kubwa kwenye soko la muziki Marekani na la dunia kwa ujumla bado kuna vingi kuhusu msanii huyu ambavyo mashabiki wake wangependa kuvijua.

Nimechukua time na kukusanya vitu vitano ambayo pengine umeshawahi kukutana navyo au hujawahi kabisa kuvisikia kuhusu Shakira… kwa mfano, unafahamu sababu kubwa iliyomsukuma Shakira kujua jinsi ya kukata kiuno? Uwezo wake kiakili je? kwanini hapendi kucheza movie yoyote kubwa ya Hollywood?

shakira7

Yote ninayo hapa chini kwenye hii list ya‘5 Things You Didn’t Know About Shakira..’ :

  1. Shakira ana uwezo wa akili wa IQ 140  huku utafiti wa kisayansi unaonyesha kuwa uwezo wa akili kwa binadamu yoyote yule sio chini ya IQ 100, hivyo Shakira ni miongoni ya watu wanaohesabika kuwa na akili sana.

Shakira4

2. Alipokuwa shule ya msingi mwalimu wake wa kwaya alimzuia staa huyo kujiunga na kwaya ya shule baada ya kumwambia mwanafunzi huyo kuwa ana sauti mbaya, na hapo ndio ilikuwa mara ya mwisho kwa Shakira kujaribu kuimba mbele za watu mpaka badaaye sana.

shakira2

3. Bibi yake Shakira upande wa mama ndiye aliyemfundisha staa huyo kukata kiuno ikiwa  ni sehemu ya asili na utamaduni wao wa kiarabu.

Shakira1

4. Shakira sio kama mastaa wengine ambao hupenda kukuza majina yao kwa kujihusisha na uigizaji wa movie, yeye yupo tofauti na wengine kwani hapendi kucheza movie kubwa za Hollywood kutokana na woga wake wa kuamini kuwa ana kiingereza kibaya.

shakira6

5. Licha ya woga wake wa kucheza movie za kiingereza staa huyo ana uwezo wa kuzungumza lugha tano kwa ufasaha, lugha hizo ni; Kifaransa, Kispania, Kiitaliano, Kireno na Kiingereza.

No comments:

Post a Comment