Thursday, 3 December 2015

Moto wa Waziri Mkuu Majaliwa unaendelea, kayakuta mengine tena bandarini Dar leo..

Hii inakuwa mara ya pili kukutana na taarifa ya ziara ya ghafla iliyofanywa na Waziri Mkuu mpya wa Tanzania, Majaliwa Kassim Majaliwa… mara ya kwanza ilikuwa siku chache zilizopita ambapo aligundua upotevu wa makontena 349, watu 12 wakakamatwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi.

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim

Waziri Mkuu Majaliwa Kassim

Kituo cha ITV kimeripoti kuwa Waziri Mkuu huyo amefanya tena ziara ya ghafla bandarini Dar pamoja na Shirika la Reli TRL na kubaini ubadhirifu mwingine, ya leo inahusu upotevu wa makontena mengine 2431 !!

No comments:

Post a Comment