Usiku wa December 2 ilikuwa ni zamu ya kuchezwa kwa mechi za Copa del Rey nchini Hispania, michezo nane ilichezwa usiku wa December 2 ila mchezo uliyochezwa mapema zaidi ni mchezo kati ya FC Barcelona dhidi ya Villanovense uliyopigwa katika dimmba la Nou Camp.
Kwa sasa FC Barcelona unaweza kuita ndio timu inayoongoza kwa safu bora ya ushambuliaji kutokana na ushindi wa mechi zao za hivi karibuni kuibuka na ushindi wa idadi kubwa ya magoli, matokeo ya mechi zao nne zilizopita zinaonesha kuwa walimfunga Real Madrid 4-0 LALIGA, wakamfunga AS Roma 6-1 UEFA, wakamfunga Real Sociedad 4-0 na usiku wa December 2 wameifunga Villanovense goli 6-1 katika mchezo wa Copa del Rey.
Kwa takwimu hizo FC Barcelona wanakuwa wamefunga jumla ya 20 ndani ya mechi nne ambapo ni wastani wa goli 5 kwa kila mechi, magoli ya FC Barcelona yamefungwa na Daniel Alves dakika ya 4, Sandro Ramirez dakika ya 21, 31, 69 na Munir El Haddadi dakika ya 51 na 76 wakati goli pekee la Villanovense lilifungwa na Juanfran dakika ya 29.
Video ya magoli ya FC Barcelona Vs Villanovense



No comments:
Post a Comment