Monday, 16 November 2015

Rais JPM Bandarini, Lowassa, Seif waitesa CCM, TPA yapunguza watu 30 + Mashine za MRI?

Good Morning mtu wangu, Uchambuzi wa magazeti redioni umekupita? Kazi yangu siku zote ni kuhakikisha zile zote kubwa za siku zinakufikia, hizi ni baadhi ya stori zilizoguswa kwenye Uchambuzi redioni.

Rais John Magufuli atua Bandarini, TPA yapunguza watendaji 30, pepo la ukwepaji kodi lafika mwisho, Mashine za kipimo cha MRI zaharibika tena Muhimbili, Edward Lowassa Seif awatesaCCM, wachimbaji waokolewa baada ya kufukiwa ardhini kwa siku 41 na nyumba 45 za bomolewa Dar es salaam, Kurasini.

Wiki moja baaada ya kutengenezwa kwa mashine za MRI katika Hospitali yaMuhimbili, mashine hizo zaharibika tena katika hospitali hiyo jana baada ya kuwahudumia wagonjwa 21… BAVICHA imetoa siku tatu kwa jeshi la polisi kuwafikisha Mahakamani wale wote waliohusika kwenye mauaji ya Mwenyekiti wa CHADEMAGeita.

Baada ya kufanya matembezi kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kukagua mashine za MRIRais John Magufuli amefanya ziari nyingineBandarini na kukagua mashine za kupima mafuta na kisha kuzitaka zianze kufanya kazi, awali zilizokuwepo zilikatazwa na wakala wa vipimo WMAkutumika kwa madai ya kuwa zinawapunja wateja.

Wakati Bunge la 11 likitegemea kuanza vikao vyake leo, kuna taarifa ya kuwepo kwa kile kinachodaiwa kuwa mvutano wa chini chini baina ya Waubunge wa CCM na Rais Dk. John Magufulikuhusu nani anaestahili kupitishwa kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Spika huku Job Ndugai apitishwa bila kupingwa… Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWAwamemteua, Goodluck Ole Medeyekutoka CHADEMA kusimama katika nafasi ya uspika.


No comments:

Post a Comment