Staa wa movie kutoka Hollywood Jean-Claude Van Dammemkali ambaye amewahi kutamba na movie kadhaa November 19 alipata nafasi ya kutembelea mazoezi ya klabu yaManchester City. Staa huyo wa Hollywood yupo jijini Manchester kwa ajili ya shughuli ya ‘black-tie dinner’ ambapo atapata nafasi ya kuoneshwa kwa movie zake.
Jean-Claude Van Damme ambaye ana umri wa miaka 55 alivyotembelea mazoezi ya Man City mastaa wa klabu hiyo hawakuacha kuchukua kumbukumbu zao kwa kupiga picha na staa huyo, wachezaji wa Man City kama Yaya Toure, Vincent Kompany, Kevin De Bruyne, Sergio Aguero pamoja na kocha wao Manuel Pellegrini hawakusita kupiga picha na Van Damme.
Mkali huyo wa movie duniani ambaye kwa miaka ya karibuni ametamba katika tangazo la bia, amewahi kutamba katika movie za mapigano zikiwemo Bloodsport, Hard Target na Universal Soldier. Hizi ni baadhi ya pichaz zake alivyotembelea Man City.

Universal Soldier hii ni movie aliyotamba nayo miaka ya 1990 aliyoicheza Jean-Claude Van Damme alicheza pamoja na Dolph Lundgren







No comments:
Post a Comment