November 21 mechi za Ligi Kuu Uingereza zimeendelea tena baada ya kusimama kwa siku kadhaa ilikupisha mechi za kimataifa, michezo kadhaa imepigwa katika viwanja mbalimbali, klabu ya Chelsea inayofundishwa na kocha Jose Mourinho ilikuwa na kibarua kigumu cha kuanza kutafuta ushindi dhidi ya klabu ya Norwich Citykatika dimba lake la nyumbani Stamford Bridge.
Mechi hiyo ambayo kwa Chelseailikuwa ya 13 ya Ligi Kuu Uingerezatoka kuanza kwa msimu huu, ikiwa ishacheza mechi 12 na kushinda 3, imefungwa 7 na kutoa sare mechi 2 haikuwa rahisi kupata matokeo licha ya kuwa ilikuwa katika uwanja wake wa nyumbani wa Stamford Bridge London kwani walikosa nafasi kadhaa za kufunga.
Hadi dakika 90 zinamalizika Chelseawalifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 licha ya kukosa nafasi kadhaa, goli la Chelsea lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayekipiga katika klabu hiyo Diego Costa dakika ya 64 ya mchezo na kuwatuliza mashabiki wa Chelsea waliokuwa hawana furaha kutoka na mfululizo wa matokeo mabovu.
Matokeo ya mechi nyinine za Ligi Kuu Uingereza Zilizochezwa November 21
- Watford 1 – 2 Manchester United
- Everton 4 – 0 Aston Villa
- Newcastle United 0 – 3 Leicester City
- Southampton 0 – 1 Stoke City
- Swansea City 2 – 2AFC Bournemouth
- West Bromwich Albion 2 – 1 Arsenal
Video ya magoli ya mechi ya Chelsea Vs Norwich City
Video ya mago ya mechi ya Watford Vs Manchester United
Magoli ya mechi ya West Bromwich Albion Vs Arsenal


No comments:
Post a Comment