Wednesday, 18 November 2015

Diamond Platnumz na Patrick Ngowi kwenye list ya Waafrika 10 Mabalozi wa Tuzo za #TFAA2015

Najua ukianza kutaja list ya Tuzo ambazo mastaa wengi wamekuwa wakiingizwa kushiriki na kushindania, huenda jina la Tuzo za TFAA sio jina ambalo umelisikia mara kwa mara.

The Future Awards Africa (TFAA) ni Tuzo ambazo hutolewa kila mwaka kwa vijana wenye umri kati ya miaka 18-31 waliofanya vizuri kwa kipindi cha mwaka husika, Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2004 na vijana wa Nigeria na mwaka 2015 zinatimiza miaka 10 ambapo kwenye list ya vijana waliotajwa kama Mabalozi waliowahi kushinda Tuzo hizo kwenye kipindi cha miaka 10, majina ya Watanzania wawili nayo yamo, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz na Patrick Ngowi.

 

Dimdond

Diamond Platnumz.

PATRICK

Patrick Ngowi.

 List ya Mabalozi wote 10 waliowataja hii hapa

Bukola ‘Asa’ Elemide – Msanii wa muziki toka Nigeria

Michel ‘Don Jazzy’ Ajere – Producer wa muziki na msanii pia kutoka Nigeria

Tara Fela Durotoye – Mrembo kutoka Nigeria

Ndindi Nwuneli – Mwanzilishi wa Taasisi ya LEAP Africa iliyopo Nigeria

Nnaemeka Ikeguonu – Mjasiriamali wa masuala ya Kilimo Nigeria

Sangu Delle – Mwanaharakati kutoka Ghana

Patrick Ngowi – Mjasiriamali wa masuala ya nishati ya umeme wa jua kutoka Tanzania

Diamond Platinumz – msanii wa muziki kutoka Tanzania 

Fogblanbenchi Lily Haritu – Mwanaharakati kutoka Cameroon

Oramait Alengoil – Mbunge kutoka Uganda

Kama unahitaji kuifahamu zaidi TFAA Awards unaweza kuingia hapa mtu wangu >>> TFAA


No comments:

Post a Comment