
Hit maker wa singo kadhaa ikiwemo ya Shauri Zao staa kutoka Morogoro Abednego Damian aka Belle 9 amekubali kushare na Bongo Fleva ya Clouds FM kwenye kipengele cha Bong0 5 kubwa kuliko kuhusu muziki wake ambao amedumu nao kwa zaidi ya miaka 7 sasa.
Belle 9 aliulizwa
kwamba anaamini kutotoa video zake kwa muda muafaka kunaangusha muziki
wake?? Kwenye jibu lake amesema ni kweli japo sio kwa asilimia kubwa kwa
sababu sio nyimbo zote alichelewesha kuzitolea video.
Kwenye sentensi nyingine Belle 9 amesema kuna video ziliwahi kutoka ila kuna nyingine zilichelewa, kwa mfano video ya wimbo wa #Amerudi akasema ile ilichelewa pamoja na video ya wimbo wa #VitaminMusic ambao alimshirikisha Joh Makini.
No comments:
Post a Comment