Januari 13: Ajali ya treni ya Mizigo ilitokea maeneo ya stesheni ya
Pugu Mpiji mabehewa matatu ya treni ya hiyo iliyokuwa ikitoka Dar es
Salaam ikielekea Bara yaliacha njia na moja kuanguka.
Februari
19: Watu wawili walikufa papo hapo huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya
basi la abiria la Kidia lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda
Mwanza kugongana uso kwa uso na lori katika kijiji cha Vikonje wilayani
Chamwino mkoani Dodoma.
Aprili 17:
Watu 38 walipoteza maisha katika matukio mawili tofauti, likiwamo la
ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace iliyoua watu 19 wakati ikifanya
safari ya wizi mkoani Mbeya.
Aprili 12: Watu 18 waliteketea kwa
moto baada ya basi la Kampuni ya Nganga Express na lori aina ya Fuso
kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya
Uduzungwa, Morogoro.
Machi 3: Watu 38 walifariki dunia na
wengine zaidi ya 60 kujeruhiwa vibaya kufuatia mvua kubwa ya mawe
iliyonyesha usiku kucha na kusababisha mafuriko katika Kijiji cha
Mwakata, Kata ya Isaka Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Aprili
6: Watu watano walifariki dunia papohapo katika kijiji cha Shilabela,
kata ya Bwanga wilayani Chato, Geita baada ya kupigwa na radi wakati
wakiendelea na ibada ya Sikukuu ya Pasaka.
Mei Mosi: Watu
wanaoshukiwa kufanya vitendo vya ugaidi walilipua bomu na kusababisha
watu watano kujeruhiwa wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa, kilichoko Kata ya Sanje
wilayani Kilombero
Mei 4: Mgomo wa madereva nchini kote ambao
kwa mara ya kwanza ulisababisha mabasi yote kutoka Dar es Salaam kwenda
mikoani na nchi jirani kushindwa kuondoka.
No comments:
Post a Comment